1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mawaziri wa G7 waahidi kuachana na mafuta ya visukuku

16 Aprili 2023

Kundi la mataifa ya G7 limeahidi kuachana mara moja na matumizi ya mafuta ya kisukuku na kuyatolea wito mataifa mengine kufuata mkondo huo.

https://p.dw.com/p/4Q9wF
Preisobergrenze für den Verkauf von russischem Diesel
Picha: Michael Probst/AP/picture alliance

Pamoja na hatua hiyo, kundi hilo limeshindwa kukubaliana juu ya ukomo wa matumizi ya vyanzo vya nishati vinavyochafua hali ya hewa, kama makaa ya mawe.

Soma zaidi:Uchafuzi wa hewa kuongezeka tena mwaka huu 

Hatua hiyo inaashiria mgawanyiko mkubwa miongoni mwa washirika unaolenga kuleta usawa kati ya mabadiliko ya tabianchi na usalama wa nishati.

Baada ya siku mbili za mazungumzo katika mji wa Sapporo kaskazini mwa Japan, mawaziri wa mazingira na mabadiliko ya tabianchi wa G7 wameapa kuharakisha hatua za kuachana mafuta hayo ya visukuku ili kufikia lengo la kutochafua kabisa mifumo ya hewa kufuatia matumizi ya mafuta hayo ifikapo angalau 2050.   

Kundi hilo linalohusisha mataifa ya Ujerumani, Italia, Canada na Umoja wa Ulaya aidha limeahidi kwa mara ya kwanza kumaliza uchafuzi mpya wa mazingira utokanao na taka la pastiki ifikapo mwaka 2040.