1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaAsia

Mawaziri wa biashara Marekani, China wakutana

28 Agosti 2023

Waziri wa Biashara wa Marekani, Gina Raimondo, amekutana na mwenzake wa China katika mkutano muhimu wa kuimarisha uhusiano kati ya mataifa hayo mawili yenye nguvu kubwa kiuchumi ulimwenguni.

https://p.dw.com/p/4Vdd9
China | Gina Raimondo in Peking
Picha: Andy Wong/REUTERS

Raimondo alikutana na Waziri wa Biashara wa China, Wang Wentao, na kuzungumzia juu ya uhusiano wa kiuchumi baina ya madola hayo mawili.

Raimondo alisema pande hizo mbili zimeanzisha mchakato wa kubadilishana taarifa mpya na vikosi kazi vitakayowawezesha kuwa na uhusiano wenye manufaa kwa pande zote.

Soma zaidi: Marekani yasaka kuimarisha mazungumzo ya kibiashara kati yake na China

"Na, kwa kweli, hiki ndicho ulimwengu unakitarajia chini ya utawala wa Rais Biden." Aliongeza waziri huyo wa biashara wa Marekani.  

Licha ya kukiri kuwa kuna hali ngumu ya uhusiano baina ya mataifa yao, lakini Raimondo alimueleza Wang kwamba wangelihakikisha wanapiga hatua kama watakuwa wawazi na kutendea kazi makubaliano yao.

Ziara yake ni sehemu ya mlolongo wa ziara za maafisa wa ngazi za juu wa Marekani nchini China katika miezi ya karibuni, inapojaribu kupunguza mvutano wa kibiashara na China.