1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaHaiti

Kiongozi wa wahalifu Haiti aahidi kuendeleza mapambano

14 Machi 2024

Kiongozi wa genge la wahalifu na mwenye ushawishi mkubwa nchini Haiti ameahidi kuendeleza mapambano yaliyolitumbukiza taifa hilo katika machafuko.

https://p.dw.com/p/4dUPA
Kiongozi wa magenge ya uhalifu Jimmy "Barbecue" Cherizier
Kiongozi wa mtandao wa magenge ya uhalifu na polisi wa zamani wa Haiti Jimmy "Barbecue" Cherizier, amesema ataendeleza mapambano nchini humoPicha: REUTERS

Kiongozi wa magenge ya uhalifu Jimmy Cherizier maarufu kama "Barbecue," amesema jana Jumatano kwamba muungano wake wa magenge yenye silaha "haujali juu ya kujiuzulu kwa Waziri Mkuu Ariel Henry."

Henry aliachia ngazi baada ya mkutano wa dharura siku ya Jumatatu na nafasi yake kuchukuliwa na Baraza Tawala la mpito.

Barbecue aliyekuwa afisa wa polisi amesisitiza kwamba wataendeleza mapambano ya ukombozi wa Haiti.

Haiti haijafanya uchaguzi wa kitaifa tangu 2016, na hakuna bunge wala rais. Nafasi ya Rais Jovenel Moise, aliyeuawa 2021, haijajazwa na Henry amekuwa akiongoza nchi hiyo tangu kifo chake.