Nchi za Ghuba zimejiandaaje baada ya biashara ya mafuta?
24 Novemba 2023Mchakato wa kimataifa wa kuhamia kwenye nishati mbadala unaweza kuonekana kuwa kifo cha kiuchumi kwa eneo la Ghuba, ambapo akiba ya mafuta ni mkondo wa utajiri usio na kikomo.
Lakini nchi hizo zenye akiba kubwa ya mafuta kuliko kwingineko kote duniani, zinakubali ukweli kwamba haiwezekani kuikwepa njia ya kuondokana na nishati za mazoea ambazo ni mafuta na gesi.
Nchi kadhaa pamoja na Saudi Arabia, Umoja wa Falme za Kiarabu na Qatar zinajenga viwanda vikubwa vya niashati endelevu wakati ambapo pia zinajiondoa kwenye nishati za hewa chafu.
Kwa mfano Qatar imejenga mtambo wa nishati ya jua wenye uwezo wa kukidhi mahitaji yake ya nishati kwa asilimia10.
Umoja wa Falme za Kiarabu ambayo mwaka huu ni mwenyeji wa mkutano wa Umoja wa Mataifa juu ya mabadiliko ya tabia nchi inajenga mtambo wa nishati ya jua, utakao kuwa mkubwa kuliko mwingine wowote duniani.
Soma pia:Viongozi wa Afrika wakutana kujadili masuala ya mazingira
Miradi kama hiyo itaiwezesha Saudi Arabia kulifikia lengo lake la kuzalisha hadi asilimia 50 ya mahitaji yake ya nishati ya umeme kwa kutumia nishati endelevu hadi kufikia mwaka 2030 na pia itauwezesha Umoja wa Falme za Kiarabu kuzalisha mahitaji yake ya nishati ya umeme kwa asilimia 44 hadi itakapofikia mwaka 2050.
Hata hivyo kwa sasa Umoja wa Falme za Kiarabu na Saudi Arabia bado zimesimama pamoja na mataifa mengine ya eneo la ghuba, yaliyomo miongoni mwa nchi 15 zinazozingatiwa kuwa wachafuaji wakubwa wa mazingira.
Qatar ndiyo inayoongoza miongoni mwa nchi hizo. Kwa wastani Qatar inatoa tani 35.59 za hewa Ukaa kwa kila mtu.
Ujerumani inatoa, wastani tani 8.09 za hewa chafu kwa kila mtu.
Mpango huo unalenga kuokoa mazingara?
Profesa mshiriki, Mohammad Al-Said anayefanya utafiti kwenye chuo cha Qatar cha maendeleo endelevu, amesema nchi za ghuba zinasonga mbele haraka katika kutekeleza malengo yao kabambe ya kueleka kwenye nishati endelevu.
Hata hivyo profesa Al Said ameeleza kuwa mchakato huo haufanyiki kwa ajili ya kuyalinda mazingira tu, bali ameeleza lengo la kuziuza nishati za mafuta na gesi ili kuchuma faida kwa kiwango kikubwa kabisa.
Mnamo mwaka 2020 Saudi Arabia ilikuwa nchi ya nne duniani katika matumizi ya mafuta na ilikuwa ya sita duniani katika matumizi ya gesi.
Soma pia:Korea Kusini huenda ikarejea kwenye nishati ya nyuklia
Licha ya kuongezeka kwa joto na vipindi vya mara kwa mara vya hali mbaya sana ya hewa, mahitaji ya mafuta yanatarajiwa kuongezeka hadi mwaka 2040.
Na ikiwa mahitaji yatapungua, mafuta yataanguka thamani. Nchi zitaweza kuvutia vitega uchumi kwa kiwango kikubwa ,ikiwa zitahamia kwenye uchumi wa nishati endelevu.
Katika juhudi za kuendeleza biashara ya kuuza gesi na mafuta na wakati huo huo kujaribu kupunguza athari za mabadiliko ya tabia nchi, mataifa ya ghuba yanalenga shabaha ya kunasa na kuhifadhi hewa ukaa.
Wanaharakati watilia shata mpango
Wanaharakati wa ulinzi wa mazingira wana mashaka juu ya utaratibu huo kwa sababu wanahoji kwamba utaratibu wa kunasa na kuhifadhi hewa chafu siyo jawabu la kweli.
Hadi sasa imewezekana kunasa chini ya asilimia 0.1 kutoka kwenye tani milioni 43.
Hata hivyo tekinolojiahiyo itazungumziwa sana kwenye mkutano wa mataifa juu ya mazingira unaofanyika kwenye Umoja wa Falme za kiarabu.
Umoja wa Ulaya unapinga utaratibu huo na badala yake unasema mkazo unapaswa kuwekwa katika kuziondoa nishati za gesi na mafuta.
Soma pia:Umeme wa Jua, nishati mbadala Barani Afrika
Miito inatolewa kwa Saudi Arabia ya kuitaka iachane na nishati chafu na badala yake itumie teknolojia za kisasa ili kuhamia kwenye nishati endelevu.Nchi za ghuba zinafanya mabadiliko.
Zinatambua kwamba bomba la fedha wanalotegemea linaaza kuzibika. Kupungua kwa mahitaji ya mafuta kutaathiri mapato ya nchi hizo.
Akiba ya fedha ya nchi hizo inaweza kuyeyuka mnamo muda wa miaka 15 endapo mahitaji ya mafuta yatapungua duniani.