1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mashirika yaunga mkono ombi la UN la dola bilioni 7

24 Mei 2023

Mashirika ya misaada yaunga mkono ombi la UN la dola bilioni 7 kwa mzozo wa Pembe ya Afrika.

https://p.dw.com/p/4Rk0E
Äthiopien | Vereilung von Hilfsgütern
Picha: Mulugeta Ayene/AP/picture alliance

Mashirika ya kiutu yanatoa wito wa ufadhili kamili wa ombi la Umoja wa Mataifa la dola bilioni 7 kwa ajili ya eneo la Pembe ya Afrika wakati wa mkutano wa kutoa ahadi unaoanza leo.

Mashirika hayo yanataja mzozo unaoongezeka na haja ya uingiliaji wa dharura ili kuokoa maisha.

Umoja wa Mataifa unasema eneo hilo linakabiliwa na ukame mbaya zaidi kuwahi kushuhudiwa katika miaka 40, huku zaidi ya watu milioni 43.3 wakihitaji msaada nchini Somalia, Ethiopia na Kenya na zaidi ya nusu ya wale wanaokosa chakula cha kutosha.

Umoja wa Mataifa unaandaa leo mkutano wa ngazi ya juu katika makao makuu yake mjini New York, ambapo mataifa wanachama na washirika watahimizwa kutoa ahadi ya msaada wa kifedha kwa mzozo wa eneo la Pembe ya Afrika.

Mashirika ya kiutu yanasema muda unayoyoma kwani jamii zilizoathirika zimeishi kwa miezi kadhaa bila chakula cha kutosha au hata chakula chochote kabisa.