MigogoroUlaya
Watu 6 wafariki Ukraine kufuatia mashambulizi ya Urusi
6 Aprili 2024Matangazo
Gavana wa Kharkiv Oleh Syniehubov amesema mashambulizi ya makombora kwenye jiji hilo yameharibu majengo ya makazi, kituo cha mafuta, shule ya chekechea, mkahawa, maduka na magari.
Urusi pia ilirushwa droni 32 za Shahed pamoja na mamkombora mengine sita usiku wa kuamkia leo, amesema kamanda ya jeshi la anga la Ukraine Myloka Oleshchuk kwenye taarifa yake.
Jeshi la Urusi hata hivyo halijasema chochote kuhusiana na mashambulizi hayo, lakini limesema kwamba Ukraine iliwafyatulia marekoti 10 aina ya Vampire mapema hii leo, ingawa walifanikiwa kuyadungua yote katika mji wa mpakani wa Belgorod kwa kutumia mifumo yake ya ulinzi wa anga.