Mashambulizi ya Ukraine yaua watu 28, Kherson na Luhansk
8 Juni 2024Mashambulizi ya Ukraine katika mikoa inayokaliwa na Urusi ya Kherson na Luhansk, yamesababisha vifo vya takribani watu 28 kwa mujibu wa maafisa wa mikoa hiyo wanaoungwa mkono na Moscow.
Gavana wa mkoa wa Kherson Vladimir Saldo amenukuliwa na Shirika la habari la Urusi, TASS, akisema kuwa vikosi vya Ukraine, kwanza vilishambulia mji huo kwa bomu lililotengenezwa na Ufaransa, kisha kushambulia tena kwa kombora la HIMARS lililotolewa na Marekani.Ukraine yaamuru watu kuhamishwa maeneo ya mkoa wa Donetsk
Ukraine na Urusi zote zimeendelea kushambuliana kwa droni katika mashambulizi ya usiku kucha.Droni zipatazo 25 za Ukraine zimeripotiwa kudunguliwa katika mikoa ya kusini mwa Urusi ya Kuban na Astrakhan, mkoa wa magharibi wa Tula na Rasi ya Crimea.
Ukraine pia imedai kudungua Droni 9 kati ya 13 za Urusi katika mikoa yake ya Poltava, Zaporizhzhia, Dnipropetrovsk na Kharkiv.