1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroUlaya

Ukraine yaamuru watu kuhamishwa maeneo ya mkoa wa Donetsk

6 Juni 2024

Ukraine imeamuru kuhamishwa kwa watoto na walezi wao kutoka miji na vijiji kadhaa katika eneo la mashariki la Donetsk, ambako mapigano na Urusi yanazidi kupamba moto.

https://p.dw.com/p/4gkIG
Mashambulizi Ukraine
Hali ya usalama katika eneo la Donetsk inazidi kuzorota, na nguvu ya makombora inaongezeka.Picha: Narciso Contreras/Anadolu/picture alliance

Gavana wa mkoa wa Donetsk, Vadym Filashkin, amesema hatua hiyo ni uamuzi muhimu uliochukuliwa, kimsingi kuokoa maisha ya watoto. Filashkin amesema hali ya usalama katika eneo hilo inazidi kuzorota, na nguvu ya makombora inaongezeka.

Miongoni mwa miji ambayo raia wanatakiwa kuondoka ni pamoja na mji wa Lyman, ambao ulishikiliwa kwa muda mfupi na vikosi vya Urusi kabla ya kuchukuliwa tena, pamoja na vijiji vingine kadhaa karibu na uwanja wa mapigano, kikiwemo kitongoji cha Progres.

Soma pia: Ukraine yadai kuzuia mkururo wa mashambulizi ya Urusi

Rais Volodymyr Zelensky amesema jeshi la Urusi sasa limejikita katika eneo la Donetsk, ambalo Kremlin ilidai kuliteka mwaka 2022, licha ya kutokuwa na udhibiti kamili wa eneo hilo.