Maashambulizi ya anga yaendelea Sudan
12 Mei 2023Matangazo
Jeshi rasmi la serikali na wanamgambo wa RSF wameshindwa kukubaliana kusitisha mapigano licha ya kuahidi kuwalinda raia na kuruhusu kupisha misaada ya kibinadamu. Kile kilichoitwa tamko la kanuni za makubaliano kilisainiwa jana jioni mjini Jeddah nchini Saudi Arabia baada ya mazungumzo ya takriban wiki moja kati ya pande hizo mbili, ingawa hakuna upande hata mmoja ambao mpaka sasa umetowa taarifa ya kuyatambuwa makubaliano hayo. Makubaliano hayo yaliyosainiwa jana yametokana na mazungumzo yaliyosimamiwa na Saudi Arabia na Marekani na yanajumuisha ahadi za pande zote mbili kuruhusu raia, wataalamu wa afya, na misaada ya kibinadamu pamoja na kupunguza madhara kwa raia na majengo ya umma.