1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaSudan

Mashambulizi ya anga yautikisa mji mkuu wa Sudan Khartoum

Daniel Gakuba
8 Mei 2023

Mashambulizi makali yameshuhudiwa Khartoum Sudan, licha ya mazungumzo ya amani yanayoendelea Saudi Arabia kutuliza machafuko.

https://p.dw.com/p/4R3dy
Sudan Khartum | Kämpfe, Rauch
Picha: Ahmed Satti/Anadolu Agency/picture alliance

Mashambulizi hayo yamejiri wakati mazungumzo ya kutafuta amani yanayofanyika katika mji wa Jeddah nchini Saudi Arabia yakishindwa kuzaa matunda.

Mwanadiplomasia wa Saudi Arabia amesema kuwa majadiliano hayo yameshindwa kupiga hatua, kwa sababu kila upande katika mzozo wa Sudan unaamini unaweza kushinda.

Akizungumza na shirika la habari la AFP kwa masharti ya kutotajwa jina, mwanadiplomasia wa Saudi Arabia amesema kuwa usitishaji mapigano wa kudumu sio mojawapo ya ajenda zinazojadiliwa.

Uhasama wa kutumia zana kali za kivita uliozuka Aprili 15 umewafanya wageni na wenyeji kuihama Sudan, kwa kutumia njia za anga na nchi kavu, kuelekea Misri, Chad, Sudan Kusini na nchi nyingine jirani.