Marekani yataka Rwanda iwaadhibu askari kwa shambulizi Kongo
7 Mei 2024Matangazo
Siku ya Ijumaa, Wizara ya Mambo ya Nje ilivishutumu waziwazi vikosi vya Rwanda kwa kuungana na waasi wa M23 na kuendesha mashambulizi kwenye kambi ya wakimbizi wa ndani katika viunga vya mji wa mashariki wa Goma na kusababisha vifo vya watu wasiopungua tisa.
Hata hivyo, Msemaji wa serikali ya Rwanda Yolande Makolo alijibu na kusema shutuma za Marekani ni za "kijinga,"na kuongeza kwenye mtandao wa X kwamba Rwanda ina "jeshi la kitaalamu" ambalo "halitawahi kushambulia" kambi ya watu waliokimbia makazi yao.
Soma pia: Vikosi vya SADC vyafanya msako dhidi ya M23
Kwa muda mrefu Marekani imekuwa ikisema kuwa kuna ushahidi kwamba Rwanda inawaunga mkono waasi wa M23 lakini Rwanda imekua ikikanusha vikali shutuma hizo.