SiasaRwanda
Rwanda yakanusha shutuma za Marekani kuhusu Kongo
4 Mei 2024Matangazo
Marekani ililaani vikali shambulio la hilo jana Ijumaa ambalo lilisababisha vifo vya watu wasiopungua kumi na wawili, kulingana na Umoja wa Mataifa.
Taarifa ya wizara ya mambo ya nje ya Marekani imesema shambulio hilo lilifanywa na watu kutoka kwenye eneo linaloshikiliwa na jeshi la Rwanda, RDF, pamoja na waasi wa M23. Marekani imesema ina wasiwasi sana kuhusu kujitanua kwa jeshi la RDF na kundi la waasi la M23 huko mashariki mwa Kongo.
Msemaji wa serikali ya Rwanda, Yolande Makolo, alikanusha kwamba jeshi la nchi yake lilifanya shambulizi hilo. Maloko alisema RDF ni jeshi linalofanya kazi kitaalamu na kamwe haliwezi kushambulia kambi ya wakimbizi wa ndani.