1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaIraq

Marekani yashambulia wanamgambo wanaoiunga mkono Iran

26 Desemba 2023

Marekani imefanya mashambulizi ya kulipiza kisasi nchini Iraq. Katika mashambulizi hayo yaliyofanyika katika mji wa Hilla uliopo katikati ya nchi hiyo.

https://p.dw.com/p/4aa7t
Bomu
Bomu lililopatikana katika eneo la Hilla, kilomita 80 kusini mwa Baghdad.Picha: picture-alliance/dpa

Mwanajeshi mmoja wa vikosi vinavyoiunga mkono Iran ameuwawa na wengine 24 wamejeruhiwa.

Marekani imesema vikosi vyake vimefanya mashambulizi katika maeneo matatu yanayotumiwa na makundi yanayoiunga mkono Iran katika hatua ya kukabiliana na mfululizo wa mashambulizi dhidi ya wanajeshi wa Marekani.

Soma pia: Watu 11 wauawa katika shambulio lililolaumiwa kwa wanajihadi Iraq

Katika taarifa yake, Waziri wa Ulinzi wa Marekani Lloyd Austin amesema vikosi vya Marekani vimefanya mashambulizi ya lazima kwenye vituo vitatu vinavyotumiwa na Kataeb Hezbollah na makundi washirika nchini Iraq.