1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Marekani yasema imewaua wanamgambo 37 nchini Syria

Hawa Bihoga
29 Septemba 2024

Kamandi Kuu ya Jeshi la Marekani, CENTCOM, imesema vikosi vya nchi hiyo vilifanya mashambulizi mawili tofauti nchini Syria na kuwaua wale imewataka kuwa "magaidi 37".

https://p.dw.com/p/4lD0h
Zana za kamandi ya jeshi la Marekani eneo la Mashariki ya Kati
Zana za kamandi ya jeshi la Marekani eneo la Mashariki ya Kati.Picha: Christopher Senenko/U.S. Navy/ZUMAPRESS.com/picture alliance

Miongoni mwao ni wanachama wa kundi la Dola la Kiislamu, na tawi la Al-Qaeda la Hurras al-Din.

Jeshi la Marekani limesema shambulio la Septemba 24 kaskazini-magharibi mwa Syria liliua "magaidi tisa" akiwemo kiongozi wa juu wa Hurras al-Din, Marwana Bassam Abd-al-Ra'uf.

Shambulio jengine la Septemba 16 katikati mwa Syria liliilenga kambi ya dola la kiislam IS na kuuawa watu wasiopungua 28, wakiwemo viongozi wanne wa juu, imeongeza taarifa hiyo bila kuwataja viongozi hao.

Mnamo mwezi Agosti, vikosi vya Marekani vilimuua kiongozi mwingine wa kundi la Hurrsa al-Din, Abu Abdul Rahman al-Malik, katika shambulio nchini Syria.