Viongozi 4 wa kundi la IS wauawa shambulio la Agosti Iraq
14 Septemba 2024Kamandi Kuu ya Jeshi la Marekani, CENTCOM, imesema kupitia taarifa kwenye mtandao wa X, kwamba operesheni hiyo iliwalenga viongozi wa ISIS na ililenga kuvuruga na kuvunja uwezo wa kundi hilo kupanga, kuandaa na kufanya mashambulizi dhidi ya raia wa Iraq.
Jumla ya watendaji 14 wa ISIS waliuawa, idadi hii ikiwa imerekebishwa kutoka 15 walioripotiwa awali. Wanajeshi watano wa Marekani walijeruhiwa, huku wengine wawili wakijeruhiwa baada ya kuanguka.
Viongozi wanne waliouawa walitambuliwa kuwa Ahmad al-Ithawi, kiongozi wa operesheni wa ISIS nchini Iraq; Abu Hammam, aliesimamia operesheni magharibi mwa Iran, Abu Ali al-Tunisi, alieshughulikia maendeleo ya kiufundi; na Shakir al-Issawi, alieongoza operesheni za kundi hilo Magharibi mwa Iran, kulingana na CENTCOM.