1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Marekani yamuwekea vikwazo kiongozi wa kundi la RSF

6 Septemba 2023

Marekani imemuwekea vikwazo kamanda wa Kikosi cha Dharura nchini Sudan, RSF Jenerali Hamdan Dagalo kutokana na jukumu lake katika machafuko na ukiukwaji wa haki za binaadamu.

https://p.dw.com/p/4W1aE
Mohammed Hamdan Dagalo
Kamanda wa Kikosi cha Dharura nchini Sudan, RSF Jenerali Hamdan DagaloPicha: AP/picture alliance

Marekani imemuwekea vikwazo kamanda wa Kikosi cha Dharura nchini Sudan, RSF Jenerali Hamdan Dagalo kutokana najukumu lake katika machafuko na ukiukwaji wa haki za binaadamu uliofanywa na wanajeshi wake katika mzozo baina yao na jeshi la Sudan.

Taarifa ya wizara ya fedha ya Marekani imesema imemuwekea vikwazo kamanda huyo anayeongoza kikosi cha RSF kwa tuhuma za kuongoza kundi la wanajeshi wanaohusika na mauaji ya raia wengi, mauaji ya kikabila na unyanyasaji wa kijinsia.Mapambano yaendelea Sudan licha ya mazungumzo yanayoendelea Saudia

Kulingana na taarifa hiyo iliyotolewa hii leo, chini ya vikwazo hivyo watazuia mali na vitu vyote vya Marekani vinavyomilikiwa na Dagalo.

Hii ni awamu ya kwanza ya vikwazo vinavyowalenga watu binafsi na kutangazwa hadharani na Marekani tangu kuzuka kwa mzozo huo nchini Sudan.