1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaSudan

Marekani yakamilisha kuwaondoa watu wake Khartoum

23 Aprili 2023

Marekani imekamilisha zoezi la kuwahamisha watumishi wa ubalozi wake nchini Sudan, huku mapigano makali yakiendelea kushuhudiwa kati ya jeshi la serikali na la dharura, RSF.

https://p.dw.com/p/4QSIC
Ubalozi wa Marekani kama unavyoonekana. Serikali imesema imekamilisha zoezi la kuwaondoa watumishi na familia zao.
Mapigano katika mji mkuu wa Sudan, Khartoum yamesababisha mataifa mengi ya kigeni kuwaondoa watumishi wa balozi na raia wao kutoka na usalama hafifuPicha: ASHRAF SHAZLY/AFP

Kulingana na wizara ya mambo ya nje ya Marekani, wafanyakazi wote wa ubalozi huo na familia zao wameondoka salama mjini Khartoum.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani, Antony Blinken, alisema awali kwamba shughuli katika ubalozi huo zimesimamishwa kwa muda, akiangazia usalama wa watumishi hao kufuatia mapigano hayo.

Rais wa Joe Biden pia alizungumzia hatua hiyo ya kufungwa kwa muda kwa ubalozi wake nchini humo, huku akitoa mwito wa kumalizwa kwa mapigano hayo.

Soma Zaidi: Jeshi la Sudan laruhusu raia wa kigeni na wanadiplomasia kuondolewa nchini humo kutokana na mapigano yanayoendelea.