1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
JamiiBurundi

Marekani yaitaka Burundi kuheshimu haki za binaadamu

6 Januari 2024

Marekani imeeleza kutatizwa na kauli ya Rais wa Burundi Evariste Ndayishimiye, ambaye wiki iliyopita aliwataka raia kuwapiga mawe watu wanaojihusisha na mapenzi ya jinsia moja.

https://p.dw.com/p/4av2j
Uganda l LGBTQ
Mwanaume wa Uganda anayejihusisha na mapenzi ya jinsia moja akiwa amesimama na bendera ya jamii hiyo Machi 25, 2023. Jamii kama yake inaelezea mashaka makubwa ya kuishi nchini humoPicha: uncredited/AP/picture-alliance

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani Matthew Miller amesema taifa hilo linatatizwa mno na matamshi hayo yanayowalenga Waburundi walio kwenye mazingira magumu na waliotengwa.

Miller ametoa wito kwa viongozi wa Burundi kuheshimu utu na upatikanaji sawa wa haki ya kila mwanajamii wa Burundi.

Inaelezwa kuwa maoni ya Ndayishimiye yamezidisha ukandamizaji dhidi ya jamii hiyo katika taifa ambalo tayari wanakabiliwa na ubaguzi wa kijamii na kifungo cha jela cha hadi miaka miwili iwapo watapatikana na hatia ya kujihusisha na mapenzi ya jinsia moja.