Marekani yaishinikiza Israel kufikia makubaliano vita Gaza
4 Septemba 2024Marekani imesema, umefika muda wa kufikiwa makubaliano kati ya Israel na kundi la Hamas ya kumaliza vita katika Ukanda wa Gaza. Kauli ya Marekani imetolewa jana baada ya waziri mkuu Benjamin Netanyahu kukataa kuitikia shinikizo zinazotolewa.
Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya Marekani, Mathhew Miller amesema Washington itafanya kazi katika siku zijazo pamoja na wapatanishi kutoka Misri na Qatar kushinikiza makubaliano ya mwisho yafikiwe.
Soma pia: Biden asema Netanyahu anakwamisha mapatano Gaza
Jana Jumanne, Marekani ilifunguwa mashtaka ya ugaidi na mengine dhidi ya viongozi sita wa kundi la Hamas yanayohusiana na shambulio la Oktoba 7 dhidi ya Israel, ambalo lilizusha vita vya Gaza.
Aidha, Mkuu wa ofisi ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa, Volker Turk ametowa mwito wa kufanyika uchunguzi huru, usioegemea upande na wa wazi kuhusu mateka sita, waliouwawa na miili yao kupatikana huko Gaza.