Marekani yailaani M23 kwa kuvunja usitishaji mapigano
7 Januari 2025Matangazo
Taarifa iliyotolewa jana na msemaji wa Wizara ya Mambo ya Kigeni ya Marekani, Mathew Miller, imesema kwamba kusonga mbele wa M23, kukiwemo kuutwaa mji huo wa Masisi, kunaharibu juhudi za kupatikana kwa amani mashariki mwa Kongo na pia kuwadhuru na kuwageuza raia kuwa wakimbizi.
Msemaji huyo alisema M23 wanapaswa kuacha mara moja harakati zao za kiuchokozi na kuheshimu makubaliano ya kusitisha mapigano.
Soma zaidi: Waasi wa M23 waudhibiti mji wa kimkakati wa mashariki ya Kongo
Kundi hilo linaloungwa mkono na Rwanda limechukuwa maeneo makubwa ya mashariki mwa Kongo tangu mwaka 2021, na kusababisha maafa na mzozo mkubwa wa wakimbizi.
Marekani imeitaka tena Rwanda kuondowa wanajeshi wake ndani ya ardhi ya Kongo.