1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroIsrael

Marekani yaahidi kuendelea kuisaidia Israel

23 Januari 2025

Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Marco Rubio amethibitisha tena uungaji mkono usioyumba kwa Israel, siku chache baada ya kusitishwa kwa mapigano katika Ukanda wa Gaza.

https://p.dw.com/p/4pVII
USA Washington 2025 | Präsident Trump kündigt 500-Milliarden-Dollar-Investition in KI-Infrastruktur an
Rais wa Marekani Donald TrumpPicha: Aaron Schwartz/Pool via CNP/Consolidated News Photos/picture alliance

Rubio amemuhakikishia Waziri Mkuu Benjamin Netanyahu kwamba wataendelea kuiunga mkono, katikati ya operesheni kubwa ya Israel katika mji wa Jenin, Ukingo wa Magharibi.

Soma pia: Trump aahidi kuwazuia wahamiaji kuingia Marekani 

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani Tammy Bruce amesema, Rubio amezungumza na Netanyahu kutokea Washington jana usiku na kusisitiza kwamba hicho ni kipaumbele cha Rais Donald Trump.

Aidha, amempongeza Waziri Mkuu huyo kwamba mafanikio ya Israel dhidi ya Hamas na Hezbollah na kumuomba kuendeleza bila kuchoka juhudi za kuwarejesha mateka wote waliosalia Gaza.