Marekani na Uingereza zashambulia waasi wa Yemen
12 Januari 2024Mashambulizi hayo yamefanyika mapema leo, baada ya wiki tano za mashambulizi yaliyotatiza shughuli katika Bahari ya Shamu, yaliyofanywa na waasi wa Kihouthi wanaoungwa mkono na Iran, ikiwa ni kuonyesha mshikamano na wapiganaji wa Hamas.
Televisheni ya waasi wa Kihouthi, Al-Masirah imetangaza kuwa mashambulizi hayo yameilenga kambi ya jeshi la anga, viwanja vya ndege na kambi ya kijeshi.
Soma pia: Iran yalaaniwa vikali katika kura ya Baraza la Usalama
Rais wa Marekani Joe Biden, amesema mashambulizi hayo yanalenga kuhakikisha shughuli katika Bahari ya Shamu zinafanyika kwa uhuru, na ameahidi kuchukua hatua zaidi iwapo itahitajika.
Iran imelaani mashambulizi hayo na imeonya kuwa yatachochea kukosekana kwa utulivu kwenye ukanda huo. Iran imesema pia mashambulizi hayo yanakiuka sheria ya kimataifa. Kundi la Hamas nalo limelaani vikali mashambulizi ya Marekani na Uingereza nchini Yemen.