1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Marekani kuamua kati ya Harris na Trump

5 Novemba 2024

Wamarekani baadaye leo wataamua iwapo Kamala Harris au Donald Trump ndiye anayestahili kuingia katika ikulu ya White House, katika uchaguzi unaodaiwa kuwa usioweza kutabirika.

https://p.dw.com/p/4mcMD
Marekani Pennsylvania 2024 | Kamala Harris
Mgombea urais Marekani kwa tiketi ya chama cha Democratic Kamala Harris Picha: Michael M. Santiago/AFP/Getty Images

Soma pia:Uchaguzi wa Marekani: Nini kinatokea siku ya uchaguzi na baadae?

Harris ambaye ni wa chama cha Democratic na makamu wa rais wa sasa na Trump ambaye ni mgombea wa chama cha Republican anayetafuta muhula wa pili wa miaka minne, kwa wiki hizi za mwisho wamekuwa wakizunguka kupiga kampeni katika majimbo 7 muhimu yanayodaiwa kuwa ndiyo yatakayoamua mshindi wa uchaguzi huo.

Watafiti wa kura za maoni wanasema hakuna mgombea yeyote ambaye ana uongozi mkubwa katika majimbo muhimu ya Pennsylvania, Michigan, Wisconsin, georgia, North Carolina, Nevada na Arizona.

Yeyote kati ya Trump na Harris wanaweza kushinda iwapo watapata ushindi katika majimbo kadhaa ya hayo muhimu.