SiasaGabon
Marekani yasitisha misaada isiyo ya kiutu nchini Gabon
27 Septemba 2023Matangazo
Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Antony Blinken ametangaza kusimamishwa kwa misaada hiyo ya kigeni nchini Gabon, na kusema wanafanyia mapitio ya mazingira yaliyochochea kuangushwa kwa aliyekuwa rais Ali Bongo Ondimba.
Blinken amesema kwenye taarifa kwamba hatua hiyo haitaathiri operesheni za serikali ya Marekani nchini Gabon, ingawa haikueleza zaidi ni shughuli zipi zinazofadhiliwa na Marekani zitakazoguswa na kiasi gani cha fedha kitasitishwa.
Gabon ni taifa la pili kufanya mapinduzi ya kijeshi baada ya Niger mapema mwaka huu. Marekani pia imesitisha baadhi ya misaada nchini Niger, ingawa bado haijabainisha rasmi kama kilichofanika ni mapinduzi.