Marais wa Nigeria na Kameruni kukutana Geneva
10 Mei 2005Geneva:
Marais wa Nigeria na Kameruni watakutana kesho Jumatano na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Kofi Annan na kuzungumzia juhudi za kutatua tatizo lao la muda mrefu la mpaka. Mkutano mkuu wa Viongozi kati ya Rais Paul Biya wa Kameruni na Olusegun Obasanjo wa Nigeria ni sehemu ya mazungumzo ya mara kwa mara kati ya nchi hizi mbili jirani. Nigeria na Kameruni, mwezi uliopita, zimeondoa tofauti zao kuhusu sehemu ya mpaka wao wa pamoja. Mgogoro wa mpaka huo wenye urefu wa km 1,690, uliowekwa na Wakoloni, umesababisha mapigano ya hapa na pale kati ya Wanajeshi wa nchi hizi mbili. Kameruni ikalichukua tatizo hilo hadi kwenye Mahakama ya Kimataifa ambayo mwezi wa Oktoba mwaka 2002 imetoa hukumu yake. Kameruni imepewa sehemu yenye utajiri wa mafuta ya Bakassi Peninsula.