SiasaSudan
Mapigano yazuka upya nchini Sudan
26 Aprili 2023Matangazo
Makabiliano hayo yamewalazimisha mamia ya raia na familia zao kuikimbia nchi hiyo na wengi wamekwama kwenye mpaka kati ya Sudan na Misri.
Mmoja ya wakimbizi hao Ahmed Elbadawy amesema, "Nimekuwa hapa kwenye mpaka wa Sudan kwa zaidi ya saa 14, umefungwa tangu jana usiku na hatujaweza kuvuuka. Hakuna chakula au maji na sijala kwa karibu siku mbili."
Hadi sasa watu wasiopungua 459 wameuwawa tangu kuzuka mapigano kati ya vikosi vinavyomtii mkuu wa jeshi na kiongozi wa taifa, Abdel Fattah al-Burhan, dhidi ya vile vya hasimu wake Mohamed Hamdan Dagalo anayeongoza kikosi cha wanamgambo wa RSF.