Burhan amani ya Sudan itapatikana kwa mazungumzo
22 Aprili 2023Matangazo
Kiongozi wa kijeshi nchini Sudan Jenerali Abdel Fattah al-Burhan amesema pande hasimu nchini humo zinapaswa kukaa pamoja kama taifa kutafuta namna ya kurejesha matumaini na maisha ya kawaida.Jenerali al-Burhan ameyasema hayo kutpitia kituo cha televisheni cha Al Arabiya, ikiwa ni takribani wiki moja baada ya mapigano ambayo yamesabisha vifo vya mamia ya watu.Katika taarifa yake hiyo amesikika akisema "Kila mtu anaathirika na vita hivyo." Hadi jana Ijumaa shirika la Afya Ulimwenguni WHO liliripoti kwamba watu 413 wameuwawa na wengine 3,551 kujeruhiwa tangu kuzuka kwa mapigano hayo.