1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaNigeria

Maoni: Uchaguzi wa Nigeria na mwanga wa matumaini

1 Machi 2023

Kwa demokrasia inayokomaa, uchaguzi wa Nigeria unaweza kuelezewa kuwa wa kuaminika na wa haki kidemokrasia. Lakini swali ni je, Rais mteule anawakilisha chaguo na imani ya vijana? Haya ni maoni ya Abdullahi Tanko Bala

https://p.dw.com/p/4O7sV
Standbild Video | Tinubu: 'We anchor well under President-elect Bola Ahmed Tinubu
Picha: APTN

Katika chaguzi zote sita zilizopita misukosuko mingi iliyojitokeza katika uchaguzi inaashiria uaminifu. Matukio ya wagombea wakubwa kushindwa katika ngome zao hayakudhaniwa hapo awali.

Soma pia: Baada ya kushinda urais, Tinubu ahimiza mshikamano Nigeria

Vyama vya upinzani vimepata mafanikio katika maeneo mengi miongoni mwa wagombea wote. Kwa ujumla kumeshuhudiwa kiu kubwa ya mabadiliko ya wagombea miongoni mwa wapiga kura na hilo hakika limethibitisha haki katika demokrasia.

Kukosekana kwa shauku ya wapiga kura ni wasiwasi mkubwa katika zoezi la uchaguzi. Asilimia 18 ya walioshiriki ni idadi ndogo kulinganisha na asilimia 37 ya wapiga kura waliojitokeza katika uchaguzi uliopita.

Nigeria Obedient Bewegung
Viana Nigeria walidai enzi mpya wakati wa kampeniPicha: Flourish Chukwurah/DW

Ninataka kuamini kwamba katika baadhi ya matukio ambako wapiga kura walihamishwa kutoka kwenye vituo walikojiandikisha, hilo pengine limechangia na katika baadhi ya majimbo kulikuwa na vurugu zilizoathiri upigaji kura. Lakini kwa kiasi kikubwa, kumekuwa na kupungua kwa shauku miongoni mwa wapiga kura nchini Nigeria na sababu kubwa ni ukosefu wa imani miongoni mwa Wanigeria kuhusu zoezi la uchaguzi.

Soma pia: Peter Obi kupinga mahakamani matokeo ya uchaguzi wa rais Nigeria

Rais mteule aliibuka kutoka kwenye makubaliano ya chama cha siasa ambacho wanachama wake wana uamuzi wa kutosha juu ya mgombea. Uchaguzi mkuu pia unaweza kutajwa kuwa sawa. Kwa hivyo ninaamini Wanigeria waliompigia kura Tinubu, wanaamini kwamba umri na afya yake havitakuwa kikwazo. Kuna Wanigeria ambao wangependelea mtu mwenye umri mdogo zaidi, lakini Asiwaju Ahmed Bola Tinubu anakuja na uzoefu utakaoleta mabadiliko. Utawala ni suala gumu lenye kuhitaji ushirikiano na mtu ambaye ameshinda ana rekodi ndefu ya kuibua timu zenye kutoa matokeo chanya ingawa kwa matumaini ya tahadhari.

Nigeria Wahlen 2023/Präsidentschaftskandidat Peter Obi
Vijana walimuona Peter Obi kama mwana mapinduziPicha: Shengolpixs/IMAGO

Katika kipindi cha serikali iliyopita, watu wengi walikuwa na matumaini makubwa na Rais Buhari wakati wa kampeni. Ilibainika kuwa siasa za Nigeria ni sugu sana linapokuja suala la kuachana na mawazo yaliyoanzishwa. Kwa hivyo, mifumo mingin ya zamani imeendelea chini ya Buhari huku mingine ikizidi kuwa mbaya. Kwa mtizamo wa matumaini, inachukuliwa kuwa Rais ajaye atajifunza kutokana na mazingira ya watu kutoridhika na kuiweka nchi kwenye mwelekeo mpya. Ni haki kuwa na matumaini.

Soma pia: Tinubu mshindi uchaguzi wa Nigeria

Swali linalohitaji kuulizwa ni iwapo rais mteule Asiwaju Bola Tinubu anawakilisha chaguo na imani ya vijana ambao wanajumuisha asilimia 60 ya wapiga kura ingawa kauli yake ya kwanza ya hadharani katika kutangaza matokeo ilizingatia zaidi kipaumbele cha vijana katika serikali yake. Ninaamini kunapaswa kuwa na ugawanyaji upya wa rasilimali watu serikalini kwa uangalifu na kwa makusudi kwa ajili ya vijana. Sera inaweza kufanikisha hili. Rais anaweza kutafuta vijana bora zaidi nchini Nigeria na kuwajumuisha katika serikali yake ili watumie ubunifu wao.

Kwa namna hiyo, siasa itakuwa jumuishi zaidi na ya kuvutia kwa vijana wataalamu na itaakisi matokeo ya jumla yanayotarajiwa katika utawala.

Mwandishi: Abdullahi Tanko Bala, DW Hausa
Tafsiri: Sylvia Mwehozi