Mama pamoja na wanawe wanne wauawa Ufaransa
26 Desemba 2023Kulingana na mwendesha mashtaka wa umma, Miili yao iliyotapakaa damu ilipatikana jana Jumatatu usiku ndani ya nyumba katika mji wa Meaux, ulio takriban kilomita 40 kaskazini mashariki mwa mji mkuu, Paris.
Soma pia: Macron aagiza usalama kuimarishwa Ufaransa
Mwendesha mashtaka wa eneo hilo amesema mama huyo na binti zake wawili walichomwa visu mara kadhaa, na watoto wengine wawili wa kiume inashukiwa waliuwawa kwa kuzibwa pumzi au kwa kuzamishwa kwenye maji.
Watoto hao walikuwa na umri wa kati ya miezi 9 na miaka 10. Majirani wamewaambia wachunguzi kwamba walisikia mayowe mapema Siku ya Krismasi.
Soma pia: Shambulizi la kisu laua watu 5, makao makuu ya polisi Paris
Taarifa zinaeleza kuwa mwanamume huyo mwenye umri wa miaka 33 anafahamika kuwa na ugonjwa wa akili, aliwahi kumchoma kisu mkewe mnamo 2019 lakini hakufunguliwa mashtaka kwa sababu ya afya yake ya akili wakati huo.