Shambulizi la kisu laua watu 5, makao makuu ya polisi Paris
3 Oktoba 2019Matangazo
Maafisa wanne wa polisi wameuawa ndani ya makao makuu ya polisi mjini Paris, Ufaransa baada ya mfanyakazi mmoja aliyekuwa na kisu kushambulia makao hayo.
Inaarifiwa kuwa mshambuliaji huyo pia ameuawa. Rais Emmanuel Macron amelizuru eneo hilo la shambulizi. Sababu ya shambulizi hilo bado haijajulikana.
Idadi ya waliojeruhiwa pia haikujulikana moja kwa moja.
Kiongozi wa chama cha polisi Jean-Marc Bailleul ameelezea kisa hicho kuwa cha uhalifu na si kitendo cha ugaidi.
Eneo hilo la mkasa, lilizingirwa kwa sababu za kiusalama.