SiasaMali
Mali yaahirisha uchaguzi wa rais uliopangwa Februari, 2024
25 Septemba 2023Matangazo
Uchaguzi huo ulilenga kuwarejesha madarakani viongozi wa kiraia katika taifa hilo la Afrika Magharibi linalokumbwa na uasi wa makundi ya kigaidi.
Msemaji wa serikali ya Bamako Abdoulaye Maiga, amewaambia waandishi wa habari kuwa duru mbili za uchaguzi zilipangwa kufanyika Februari 4 na 18, 2024, zitaahirishwa kidogo kutokana na sababu za kiufundi, ambazo zinahusiana na suala la kupitishwa kwa katiba mpya mwaka huu na mapitio ya orodha ya wapiga kura.
Aidha Maiga ameelezea pia mzozo walionao na kampuni ya Ufaransa ya Idemia, ambayo utawala wa kijeshi umesema inahusika na mchakato wa kuhesabu watu.
Tarehe mpya za uchaguzi wa rais nchini Mali zitafahamishwa hapo baadaye.