SiasaMali
Serikali ya Mali yaandaa mazungumzo ya amani
27 Januari 2024Matangazo
Mkuu wa serikali ya kijeshi, Choguel Kokalla Maiga amesema kwenye mkanda wa video uliochapishwa kwenye mitandao ya kijamii jana Ijumaa kwamba hawatarudia tena kutafuta suluhu kutoka nje.
Algeria ilikuwa mpatanishi mkuu katika juhudi za kurejesha amani kaskazini mwa Mali, katika makubaliano yaliyosainiwa mjini Algiers mwaka 2015 kati ya serikali ya Mali na makundi yenye silaha ya kabila la Tuareg.
Makubaliano hayo hata hivyo yalianza kuvunjwa mwaka jana baada ya kuzuka mapigano kati ya wanaotaka kujitenga na jeshi la serikali mnamo mwezi Agosti baada ya miaka minane ya utulivu, wakati pande zote zikihangaika kuziba pengo lililoachwa na walinda amani wa Umoja wa Mataifa walioondoka.