serikali yafikia makubaliano na makundi ya wanamgambo Libya
24 Agosti 2024
Kulingana na Waziri wa Mambo ya Ndani wa Libya Imad Trabelsi pande hizo mbili zimefikia makubaliano baada ya Umoja wa Mataifa kuonesha wasiwasi kuhusu mapigano ya hivi karibuni na mzozo unaoihusu benki kuu ya nchi hiyo.
Gavana wa benki hiyo Seddik Seddik al-Kabir, amekuwa akikosolewa na watu wa karibu na Waziri Mkuu Abdulhamid Dbeibah kuhusu usimamizi wa rasilimali za mafuta na bajeti ya serikali.
Walibya wanataka mipasuko ikome mna uchaguzi ufanyike nchini mwao
Jumapili iliyopita, mkuu wa kitengo cha tehama cha benki hiyo alitekwa nyara kwa muda na kundi la wabeba silaha ambalo halikutambuliwa, hali iliyosababisha kusimama kwa shughuli za taasisi hiyo hadi alipoachiliwa.
Libya imekuwa ikipambana kujiimarisha baada ya miaka mingi ya mzozo baada ya aliyekuwa kiongozi wa nchi hiyo Moamer Ghadafi kuondolewa madarakani.
Hadi sasa taifa hilo linakabiliwa na mgawanyiko kati ya serikali inayotambuliwa na Umoja wa Mataifa inayoongozwa na Waziri Mkuu Abdulhamid Dbeibah, na utawala ulio upande wa mashariki unaoongozwa na Khalifa Haftar.