MigogoroMyanmar
Makumi ya Warohingya waokolewa baharini wakikimbia madhila
21 Machi 2024Matangazo
Boti ya mbao ya wakimbizi hao na meli nyingine iliyokuwa ikijaribu kuwasaidia zote mbili zilipinduka jana Jumatano, huku manusura wakikadiria takribani Warohingya 150 walikuwemo kwenye boti hiyo na wengi miongoni mwao walizama majini.
Kundi la waokozi walikimbilia baharini kuwaokoa wakimbizi hao baada ya kuwaona wakiwa wamekwama majini, wakishikilia mabaki ya boti iliyozama karibu na pwani ya jimbo la Aceh, mashariki mwa nchi hiyo.
Shirika la uokozi la Banda Aceh limesema jumla ya wahanga 69 wameokolewa, 42 kati yao wakiwa ni wanaume, wanawake 18 na watoto 9.
Maelfu ya Warohingya wengi wao wakiwa Waislamu wanakimbia mateso nchini Myanmar, na wengi huondoka kupitia baharini wakijaribu kufika Malaysia au Indonesia.