1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroUlaya

Makombora ya Urusi yawajeruhi raia 17 wa Ukraine

Angela Mdungu
20 Oktoba 2024

Jeshi la anga la Ukraine limearifu kuwa limeziharibu droni 31 kati ya 49 zilizoyashambulia maeneo kadhaa ya Ukraine usiku wa kuamkia Jumapili. Limeongeza kuwa droni 13 zilipoteza mwelekeo na mbili zilielekea Belarus.

https://p.dw.com/p/4m01b
Urusi na Ukraine zimeendelea kushambuliana
Sehemu ya athari za droni baada ya Ukraine kushambulia Urusi 15.10.2024Picha: Dmitry Yagodkin/TASS/dpa/picture alliance

Hayo yanajiri huku ikiarifiwa kuwa watu 17 wamejeruhiwa baada ya Urusi kuushambulia kwa makombora mji wa Kusini mwa Ukraine wa Kryvyi Rih.

Mkuu wa utawala wa jeshi wa mkoa, Oleksandr Vilkul amesema zaidi ya majengo ishirini yameharibiwa katika mashambulizi hayo yaliyoulenga pia mji mkuu Kyiv na mkoa wa magharibi wa Lviv.

Soma zaidi: Urusi yafanya mashambulizi 114 Ukraine ndani ya masaa 24

Katika hatua nyingine, Ukraine imefanya mashambulizi ya droni na kukilenga kiwanda cha kutengeneza silaha cha kijeshi ndani ya Urusi.

Wizara ya ulinzi ya Urusi imesema ilizidungua droni 110 zilizorushwa na Ukraine ikiwemo moja kwenye eneo la Moscow ambapo watu wanne wamejeruhiwa. Droni 43 ziliharibiwa katika mkoa wa Kursk na nyingine 27 Kusini magharibi mwa Lipetsk.