1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaMarekani

Mahakama ya juu Marekani yatupilia mbali kesi ya Republican

2 Novemba 2024

Mahakama ya Juu ya Marekani imetupilia mbali kesi inayohusu upigaji wa kura kwa njia ya posta iliyowasilishwa na chama cha Republican katika jimbo la Pennsylvania, siku chache tu kabla ya kufanyika kwa uchaguzi.

https://p.dw.com/p/4mVwu
 Washington
Mahakama ya juu nchini Marekani Picha: Kevin Mohatt/REUTERS

Mahakama ya Juu ya Marekani imetupilia mbali kesi inayohusu upigaji wa kura kwa njia ya posta iliyowasilishwa na chama cha Republican katika jimbo la Pennsylvania, siku chache tu kabla ya kufanyika kwa uchaguzi wa rais nchini humo.

Majaji walikataa ombi la chama cha Republican lililotaka kura zilizopigwa mapema katika jimbo hilo zisihesabiwe kwa kusema, zilikuwa na kasoro na kwamba huenda zikawa zimekipendelea chama cha Democrats. Kwa kawaida kura zilizopigwa mapema huwekwa kando na kuhesabiwa tu baada ya kuthibitishwa.

Soma zaidi. WFP yasema haitochukua jukumu la UNRWA huko Gaza

Uamuzi wa Mahakama ya Juu katika kura hiyo kwa jimbo la Pennsylvania unatajwa kuwa ni hatua muhimu hasa katika wakati huu ambapo kampeni za uchaguzi zimepamba moto. Ushindi wa kura katika jimbo hilo ni hatua muhimu katika matokeo ya uchaguzi.