1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mahakama ya EAC yajiandaa kwa rufaa ya Loliondo

Veronica Natalis
6 Februari 2023

Mahakama ya Afrika Mashariki leo imekutana katika kikao chake cha kwanza cha maandalizi ya kusikiliza rufaa ya wananchi wa Loliondo Tanzania.

https://p.dw.com/p/4N9gB
Maasai aus Loliondo in Tansania
Picha: Judith Fehrenbacher

Wanaopinga maamuzi ya mahakama hiyo yaliyotolewa mwezi septemba mwaka jana, kuhusu kuchukuliwa kwa sehemu ya eneo la ardhi na serikali ya nchi hiyo. Kikao hicho kilichokuwa baina na majaji na mawakili wa waleta maombi pamoja na mambo mengine kimepanga utaratibu wa kusikilizwa kwa shauri hilo.

SOMA PIA: Sakata la Loliondo laibuka tena bungeni Dodoma

Wakili Donald Deya, kiongozi wa jopo la mawakili wa walalamikaji amewaambia waandishi waandishi wa habari kwamba wateja wake wameomba mwezi mmoja mpaka tarehe sita mwezi Machi mwaka huu kuwasilisha hoja zao kwa maandishi, na wajibu maombi nao wameomba mwezi mmoja mpaka tarehe tano mwezi Aprili mwaka huu watawasilisha hofa zao za rufaa.

SOMA PIA: Asasi za kiraia kutoridhishwa na tathmini kuhusu Loliondo

Hayo yanakuja kufuatia maamuzi ya mahakama hiyo ya Jumuiya ya Afrika Mashariki mwezi Septemba mwaka jana 2022, kutupilia mbali maombi ya wananchi wa jamii ya wafugaji ya Maasai katika kesi iliyohusisha mgogoro wa ardhi baina ya serikali ya Tanzania na wananchi hao, ambapo  waliitaka mahakama hiyo  izuie shughuli zinazoendeshwa na serikali  za kuwaondoa kwa nguvu wao na mifugo yao mpakani mwa hifadhi ya Serengeti na pori tengefu la Loliondo, wakisema kuwa serikali imekiuka mahsarti ya mkataba wa kuanzishwa kwa jumuiya ya Afrika Mashariki. Hata hivyo nini kinatarajiwa baada ya rufaa hiyo kuanza kusikilizwa? Odero Charles Odero ni mkurugenzi wa kutetea haki za binadamu kutoka shirika la kiraia la CILA.

SOMA PIA: Maboma ya Wamasai yachomwa Tanzania

Madai mengine yanayotolewa na wafugaji wa jamii ya Maasai  ni kupinga kuchukuliwa kwa  eneo la ardhi lenye ukubwa kilometa za 1500 kutoka vijiji 14 vya wilaya hiyo na wao kuondolewa kwa nguvu, ambapo wanaeleza zoezi hilo mbali na kukiukwa kwa mkataba wa Afrika Mashariki na itifaki ya soko la pamoja, lakini pia zoezi hilo linavunja haki za binaadamu.