1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroRwanda

Korti Rwanda yamhukumu miaka 20 mtuhumiwa mauaji ya kimbari

6 Septemba 2024

Mahakama nchini Rwanda imemkuta na hatia Venant Rutunga ya kushiriki mauaji ya kimbari ya mwaka 1994, na kumuhukumu kifungo cha miaka 20 jela, hii ikiwa ni kulingana na vyombo vya habari vyenye mahusiano na serikali.

https://p.dw.com/p/4kM3h
Rwanda | Mauaji ya kimbari | Nyamata
Mafuvu ya vichwa vya binadamu yaliyohifadhiwa katika kumbukumbu ya mauaji ya kimbari huko Nyamata, ndani ya Kanisa Katoliki ambapo maelfu ya watu waliuawa wakati wa mauaji ya kimbari ya 1994 nchini Rwanda.Picha: SIMON MAINA/AFP

Venant Rutunga mwenye miaka 75, alirudishwa Rwanda kutokea Uholanzi mwaka 2021 alikofunguliwa mashitaka kuhusiana na madai kwamba aliagiza kufanyika mauaji hayo zaidi ya robo karne iliyopita.

Soma pia: Wiki ya kumbukumbu ya mauwaji ya kimbari nchini Rwanda 

Kulingana na mwendesha mashitaka, Rutunga aliwapeleka polisi kwenye taasisi ya utafiti wa kilimo kulikokuwa na wafanyakazi wa Kitutsi na watu wengine waliokuwa wamejificha, ambao wote waliuawa. Rutunga aliwahi kuwa mkurugenzi wa kikanda wa taasisi hiyo ya ISAR.

Rutunga, aliyekana mashtaka, alidai kuwa aliwaita maafisa hao ili kulinda usalama, uamuzi ambao alisema uliidhinishwa na bodi ya wakurugenzi ya ISAR.