1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mahakama Kuu DRC yaruhusu Katumbi kuwania urais

31 Oktoba 2023

Mahakama Kuu nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo imetupilia mbali kesi iliyotaka kumzuia mwanasiasa wa upinzani Moise Katumbi kuwania urais kwa madai kuwa si raia wa Kongo.

https://p.dw.com/p/4YDXN
Moise Katumbi aus DR Kongo
Moise KatumbiPicha: Nicolas Maeterlinck/BELGA/dpa/picture alliance

Kesi hiyo iliwasilishwa mahakamani na mgombea mwingine Noel Tshiani akidai kuwa Katiba ya Kongo hairuhusu uraia pacha kwa kuwa baba wa Katumbi alikuwa raia wa Italia.

Wakili wa Katumbi Herve Diakiese aliteta wakati wa kesi hiyo hapo jana kwamba hakuna uthibitisho wowote ya kuwa mteja wake ana uraia mwingine zaidi ya ule wa Kongo.

Soma pia: HRW: Serikali ya Kongo yakandamiza wapinzani kuelekea uchaguzi

Katumbi, mfanyabiashara tajiri mwenye umri wa miaka 58 na Gavana wa zamani wa Jimbo la Katanga, anachukuliwa kuwa mmoja wa wagombea wakuu dhidi ya Rais aliye madarakani Felix Tshisekedi katika uchaguzi uliopangwa kufanyika Desemba 20 mwaka huu.