1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Maduro akataa kukimbia Venezuela

10 Agosti 2024

Rais Nicolas Maduro amelikataa pendekezo la Rais Jose Raul Mulino wa Panama la kukimbilia nchi salama ili kuruhusu kipindi cha mpito cha uongozi nchini Venezuela, ambako Maduro anatuhumiwa kuiba uchaguzi wa Julai 28.

https://p.dw.com/p/4jJbK
Venezuela Nicolas Maduro
Rais Nicolas Maduro wa Venezuela akihutubia wafuasi wake mjini Caracas.Picha: Matias Delacroix/AP Photo/picture alliance

Mulino alikiambia kituo cha televisheni cha CNN cha Marekani kwamba alikuwa tayari kumkaribisha Maduro kwa muda akiwa anaelekea kwenye nchi nyengine.

Lakini Maduro amemtuhumu Mulino, ambaye mwenyewe aliingia madarakani miezi mitatu iliyopita, kwa kutumiliwa na Wamarekani. Rais huyo wa Venezuela alimuonya mwenzake wa Panama asiingilie mambo yasiyomuhusu.

Soma zaidi: Misaada ya dharura ya Marekani imekwama mpakani Venezuela

Mulino ameitisha mkutano wa kilele wa mataifa ya Amerika Kusini kuzungumzia matokeo ya uchaguzi wa Venezuela, na amedai kuwa tayari marais wenzake saba wamekubali kuhudhuria.

Mkutano huo utafanyika katika Jamhuri ya Dominika tarehe 16 mwezi huu, siku ambayo pia ataapishwa rais mpya wa jamhuri hiyo, Luis Abinader.