1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Madereva wa treni wagoma Ujerumani

Josephat Charo
10 Januari 2024

Mgomo wa madereva wa treni wa Ujerumani umesababisha huduma za usafiri wa abiria kote nchini kukaribia kukwama kabisa mapema leo asubuhi.

https://p.dw.com/p/4b3Gm
Ujerumani, Köln | Mgomo wa maderava wa treni
Vituo vya treni vikiwa vitupu kufuatia mgomo wa madereva wa treni UjerumaniPicha: Marc John/IMAGO

Shirika la usafiri wa treni Ujerumani, Deutsche Bahn limetangaza kwamba madereva wengi walianza mgomo wao mwendo wa saa nane usiku wa manane.

Mgomo wa treni za mizigo ulianza siku ya Jumanne saa kumi na mbili jioni. Mgomo huo utaendelea hadi Ijumaa jioni saa kumi na mbili jioni.

Soma pia: Ujerumani yatikiswa na mgomo wa usafiri wa Umma

Ratiba ya dharura ya safari za treni inatumika huku asilimia 80 ya huduma za kawaida za masafa marefu zikifutwa kabisa.

Deutsche Bahn imesema kutakuwa pia na athari kwa huduma za treni za masafa mafupi, ingawa upana wa athari zake utatofautiana kutoka eneo moja hadi lingine.