Madaktari Nigeria warejea kazini baada ya mgomo wa miezi 2
5 Oktoba 2021Madaktari hao wamekuwa wakipigania ongezeko la mishahara, mafao na vifaa vya kazi.
Chama cha Madaktari nchini humo, NARD, ambacho kinawakilisha asilimia 40 ya madaktari wote, kimesema, japokuwa baadhi ya masuala hayajapatiwa ufumbuzi, yale yanayohusu malipo yametatuliwa.
Kwa mujibu wa Rais wa NARD, Dare Ishaya, mgomo huo ulioanza tarehe 2 Agosti utamalizika rasmi leo na kesho saa 2:00 asubuhi, madaktari wote watarejea kazini.
Nigeria yenye wakaazi milioni 210, ina madaktari 42,000. Madaktari 16,000 kati yao ni wanafunzi wanaosemea utaalamu bingwa wa maeneo yao.
Mgomo wa mwaka huu ulifanyika wakati taifa hilo lenye watu wengi zaidi barani Afrika likipambana na janga la UVIKO-19.
Hadi sasa, watu 200,000 wameambukizwa virusi vya corona, ambapo 2,720 wamepoteza maisha.