1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Macron ziarani nchini Sweden

30 Januari 2024

Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron anafanya ziara siku ya mbili nchini Sweden kuanzia leo ambayo itatuama juu ya vita nchini Ukraine na matayarisho ya Sweden kujiunga na Jumuiya ya Kujihami ya NATO.

https://p.dw.com/p/4bqik
Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron
Rais wa Ufaransa Emmanuel MacronPicha: Ludovic Marin/AP Photo/picture alliance

Mapema leo mchana, Macron akiwa pamoja na mkewe Brigitte walilakiwa na mfalme Carl XVI kwa heshima ya gwaride la kijeshi katika hafla iliyofanyika kwenye kasri la nchi hiyo mjini Stockholm. 

Akizungumza na mfalme Carl Gustaf, Macron amesema ananuwia kuimarisha uhusiano kati ya Ufaransa na Sweden, mshikamano ndani ya Umoja wa Ulaya hasa wakati Sweden inakaribia kuingia ndani ya Jumuiya ya NATO.

Soma pia:Urusi na Ukraine zashambuliana usiku wa kuamkia leo

Anatarajiwa jioni hii kuwa na mazingumzo na waziri mkuu Ulf Kristersson na baadae watajiunga na Mfalme Gustaf kujadili hatma ya usalama barani Ulaya kwenye chuo cha kijeshi mjini Stockholm.