1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Urusi na Ukraine zashambuliana usiku wa kuamkia leo

30 Januari 2024

Ukraine imesema Urusi imefanya hujuma nzito usiku wa kuamkia leo kwa kuvurumisha makombora na kutuma ndege zisizo na rubani kuilenga miundombinu yake ya nishati na vituo vya kijeshi.

https://p.dw.com/p/4bqCB
Kyiv, Ukraine | Rais Volodymyr Zelensky
Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky Picha: Thomas Coex/AFP

Maafisa wa nchi hiyo wamemesema watu wawili wameuwawa na wengine 5 wamejeruhiwa katika mfululizo wa mashambulizi kutoka Moscow yaliyoulenga mji mkuu Kyiv na majmbo ya Dnipropetrovsk na Kharkiv

Inaarifiwa kwamba Moscow ilifyetua makombora mawili na kurusha droni 35 ambazo 20 kati ya hizo zilivuka mifumo ya ulinzi ya Ukraine.

Soma zaidi:Ukraine yashambulia uwanja wa ndege wa kijeshi huko Crimea

Serikali mjini Kyiv imewarai washirika wake wa magharibi kuisaidia kuboresha mifumo yake ya ulinzi wa anga ikisema hilo nni jambo la kipaumble kwa mwaka 2024. 

Urusi nayo kwa upande wake imesema imezidungua droni 21 za Ukrane zilizorushwa juu ya anga yake na nyingine zikiilenga rasi ya Crimea iliyonyakuliwa na Moscow mwaka 2014.