SiasaUfaransa
Macron aanzisha mazungumzo magumu ya serikali mpya Ufaransa
24 Agosti 2024Matangazo
Wiki sita baada ya uchaguzi wa haraka ambao hakuna chama kilichopata wingi wa kutosha wa viti bungeni na ambao kambi ya Macron ilipoteza hadhi yake ya kuwa kundi kubwa la kisiasa, bado hajamtangaza waziri mkuu mpya.
Soma pia: Bunge jipya ya Ufaransa kukutana Alhamisi wiki hii
Jukumu la kwanza kuu la waziri mkuu ajaye litakuwa kuwasilisha bungeni mpango wa bajeti ya mwaka ujao. Chama cha siasa za mrengo wa kushoto cha New Popular Front - NFP -- ambacho kiliibuka kuwa kundi kubwa lakini bila kupata wingi wa viti -- kimesema kinataka mchumi Bibi Lucie Castets mwenye umri wa miaka 37 awe mkuu mpya wa serikali. Lakini upande wa Macron unapendelea kuunda muungano na mrengo wa kulia.