Machafuko yaibuka tena katika mji mkuu wa Sudan
16 Julai 2023Mashuhuda wameliambia shirika la habari la AFP kuwa ndege za kivita za jeshi zilizilenga kambi za kikosi cha wanajeshi wa dharura cha RSF, mashariki na kusini magharibi mwa Khartoum ambapo kikosi hicho kilijibu mashambulizi.
Soma pia: ICC yaanzisha uchunguzi mpya katika machafuko ya Sudan
Taarifa zaidi zinasema droni za RSF zilielekeza mashambulizi katika hospitali kubwa ya jeshi mjini Khartoum. Shambulio la aina hiyo lilifanywa Jumamosi katika hospitali hiyo hiyo tukio lililosababisha vifo vya watu watano na kuwajeruhi wengine 22.
Takwimu za Umoja wa taifa zinaonesha kuwa, Hadi sasa vita kati ya Jenerali Abdel Fattah al-Burhan na aliyekuwa msaidizi wake anayekiongoza kikosi cha RSF Mohammed Hamdan Daglo vimeshasababisha vifo vya zaidi ya watu 3,000 na kusababisha wengine milioni 2.5 wayakimbie makazi yao.