Mabadiliko ya tabianchi yasababisha joto kali Sahel
18 Aprili 2024Matangazo
Kwa mujibu wa utafiti wa uliochapishwa na shirika la World Weather Attribution (WWA) siku ya Alhamisi (Aprili 18), mataifa ya Mali na Burkina Faso yalikabiliwa na wimbi la joto kali kuanzia Aprili Mosi hadi Aprili 5, ambapo viwango vya joto vikiongezeka hadi zaidi ya nyuzi 45 kwa kipimo cha Celsius na kusababisha idadi kubwa ya vifo.
Soma zaidi: Watu 11 wafa kwa kimbunga nchini Madagascar
Shirika hilo lilisema kuwa na joto kali mnamo Machi na Aprili 2024 katika eneo hilo lilitokana na walihusisha na "mabadiliko ya hali ya hewa yanayosababishwa na binadamu."
Nchi za eneo la Sahel zimekuwa zikikabiliwa na ukame tangu miaka ya 1970 pamoja na vipindi vya mvua nyingi kuanzia miaka ya 1990.