1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kimbunga Gamane chaua watu 11 nchini Madagascar

28 Machi 2024

Watu 11 wamekufa kutokana na kimbunga kilichoipiga Madagascar ambacho pia kimeangusha miti na maji ya baharini yakiingia kwenye mitaa ya taifa hilo la kisiwa.

https://p.dw.com/p/4eDs9
Picha za satelaiti zikionyesha kimbunga Freddy
Picha za satelaiti zikionyesha kimbunga Freddy kilipokuwa kikiisogelea Madagascar 20.02.2023. Madagascar imepigwa na kimbunga hivi sasa cha GamanePicha: NASA VIA REUTERS

Maafisa nchini Madagascarwamesema kimbunga hicho cha Gamane kinachokwenda kwa kasi ya chini ghafla kimegeuka na kuipiga nchi hiyo.

Haya yanafanyika huku upepo unaovuma kwa kasi ukiangusha miti na maji ya baharini yakiingia mitaani na kusomba nyumba.

Afisi ya kitaifa ya kupambana na majanga nchini humo imesema asubuhi ya leo kuwa, kimbunga Gamane kilikuwa kimekadiriwa kukivuka kisiwa hicho cha Madagascar kilicho katika Bahari ya Hindi kusini mwa Afrika, ila kilibadilisha mkondo na kupiga katika eneo la kaskazini.

Mamlaka zinasema watu sita wamezama maji na wengine watano wamefariki kutokana na kuangukiwa na miti au nyumba, huku watu elfu 7 wakiathirika na kimbunga hicho.