Mabadiliko ya tabia nchi ni kitisho cha usalama wa chakula
12 Desemba 2023Matangazo
Akizungumza pembezoni mwa mkutano wa mazingira wa COP 28 mjini Dubai, Frick amesema bado dunia ina miaka sita hadi saba ya kubadilisha muelekeo wa mabadiliko ya tabia nchi akisisitiza kuwa muda huo ukimalizika kutakuwa na matokeo yasiokuweza kurekebishwa.
Ameongeza kuwamabadiliko ya tabia nchi ni kitisho kikubwa cha usalama wa chakula. Frick amesema mfumo wa chakula ulioko sasa sio wa uzalishaji, umebakia tu kuwa wa usambazaji na hilo linatishia pia kuwa na upungufu wa chakula.
Soma pia:WFP: Njaa kali itaongezeka nchini Somalia kufuatia mafuriko
Wawakilishi kutoka mataifa 200 duniani wanahudhuria mkutano huo wa kilele katika mji wa Dubai, unaotarajiwa kumalizika leo Jumanne.