Maandamano ya kupinga chama cha AfD kufanyanika Ujerumani
11 Januari 2025Matangazo
Waandalizi wanatarajia zaidi ya watu 10,000 kuhudhuria maandamano dhidi ya AfD. Waandamanaji kutoka takriban miji 70 wanatarajiwa kuwasili katika mabasi zaidi ya 100 yaliyokodishwa kwa tukio hilo.
Hatua hiyo inafuatia kufunguliwa leo kwa mkutano wa siku mbili wa chama cha AfD huko mjini Riesa, jimbo la Saxony, mashariki mwa Ujerumani.
Waandamanaji pia walipanga kuzuia njia za ufikiaji kwenye ukumbi ambapo mkutano wa chama cha mrengo mkali wa kulia cha AfD utafanyika.
Mamlaka za jimbo la Saxony zimepeleka polisi wa kuzuiya ghasia. Uchaguzi wa bunge nchini Ujerumani unapangwa kufanyika Februari 23.